Subscribe:

Follow Us by Email

Ads 468x60px

August 01, 2012

Kocha Azam, Aachia Ngazi

Kocha wa timu ya Azam, muingereza Stewart Hall, ameachia ngazi rasmi kuifundisha timu hiyo.
Akithibitisha taarifa hiyo, Meneja wa Azam, Patrick Kahemele, alisema kuwa kocha huyo hajatimuliwa kama wengi wanavyosema bali imefikia kipindi ambacho kocha wao alihitaji kwenda kwao kupumzika na si vinginevyo.
Kwa upande wako mwenyewe, Stewart Hall alisema kuwa anashukuru amekamilisha alichotaka kukifanya ikiwemo kuiendeleza timu ya Azam, shule ya soka ya Azam na kikubwa zaidi kuisimamia Azam-Chamazi Complex. Amelikamilisha hilo na sasa inabidi arudi nyumbani baada ya kuwa hapa nchini kwa takribani miaka mitatu.
Azam inaanza mchakato wa kutafuta kocha mpya na tayari imeshapokea maombi ya walimu mbalimbali kutoka nje ya nchi.

0 comments:

Post a Comment

Page viewers