Subscribe:

Ads 468x60px

September 04, 2011

Converse All Stars na maajabu yake


Kwa mfuatiliaji mzuri sana na wa karibu wa Fashion and designs especially zinazoenda na wakati, ukimtajia "Chuck Taylors" au "Chucks" atakuelewa faster sana unazungumzia nini! Ila kuwaweka wazi raia wengi zaidi ongezea neno All Stars yani "Chuck Taylor's All Stars" moreover malizia kabisa kwa kusema "Converse AllStars" au "Cons". You dig!?

Converse All Star nia aina ya kiatu kinachojulikana kama Sports gear kwani ni aina ya viatu vya raba na convasi ambayo ni mahsusi kwa ajili ya michezo ambavyo vinatengenezwa na kampuni ya viatu ya Converse na kwa mara ya kwanza vilitengenezwa mwaka 1917

Kwanini Chuck Taylor's All Star?

Maybe ndo swali utakalokua unajiuliza. Chuck Taylor alikuwa mwanakikapu afisa mauzo wa Converse ambaye alitoa wazo wa viatu hivyo kutumika kwenye mchezo huo. Baada ya hapo akawa msemaji mkuu wa viatu hivyo na kampuni kwa ujumla na kupewa jina lake. Hiyo ilikuwa  miaka ya 1920.

Kwa zaidi ya miaka 90 sasa viatu hivyo vimezidi kujipatia umaarufu na kuvaliwa na watu wa rika na jinsia mbalimbali kutokana na kuwa na maumbo na rangi tofauti tofauti zenye kumfit na kumpenedezesha yeyote yule.

Kwa mfano viatu vya hapo juu, vinaweza kuvaliwa na mvulana, msichana hali kadhalika. Hata wazee pia hutupia All stars coz walizikuta kitambo na wazidumisha bado.

Ni Exclusive kwa Michezo tu?


Hapana! hebu take a look kwa hiyo Converse ya brown hapo juu, halafu tengeneza picha ya ukiwa na Cadet ya khaki au nyeusi na t-shirt moja ya brown au white matata sana then katiza kitaa au jitupe klabu au hata kuomba viza ubalozini moreover hata kwenye job interview, habari yake sio ndogo!

Kwa kifupi hayo ndo maajabu ya viatu hivi ambavyo bila shaka kila mtu anayekwenda na fashion atakuwa na pair zake kama tatu na zaidi hivi...Coz they keep you smart!

Fanya hivyo tuoneeeeee!

0 comments:

Post a Comment

Page viewers