Subscribe:

Ads 468x60px

April 04, 2011

Meza Moja na Ben Pol......



rokBrothers safari hii ilitia maguu hadi katika studio za M-Lab, Kinondoni kwenda kukutana na kufanya mahojiano na Mshindi wa tuzo ya Kili ya Wimbo Bora wa R&B, Ben Pol na kufunguka nae kama hivi:

HISTORIA FUPI:
Wengi tunamfahamu kama Ben Pol lakini jina lake la vitambulisho na vyeti ni Bernard Paul. Ni mtoto wa Pili kwenye familia ya watoto wanne lakini kwa bahati mbaya kaka yake alifariki hivyo kubakia watatu. Baba yake ni mzaliwa na Dodoma na mama yake ni mzaliwa wa Shinyanga. Bernard Paul ni Mgogo halisia.

ELIMU:
Alianza elimu yake ya msingi mwaka 1997 na kumaliza mwaka 2003 katika shule ya msingi Vingunguti. Mwaka 2004 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Dar-Es-Salaam sekondari na kumaliza kidato cha nne mwaka 2007, Novemba. May 2008 aliendelea na elimu yake ya juu katika shule ya sekondari Azania hadi mwaka 2010 alipomaliza kidato cha sita. Baada ya hapo hakuendelea tena na elimu yake ya chuo baada ya kuamua kujiingiza kwenye shughuli za muziki.

MUZIKI:
Ben anasema alipenda kuimba tangu shule ya msingi kwa kuimba nyimbo za watu na kukariri nyimbo zao lakini hadi kufikia kidato cha tatu mwaka 2006 alinza kujifunza kuimba nyimbo zake mwenyewe lakini kutokana na kutingwa na masomo alisubiri hadi alipomaliza kidato cha nne mwaka 2007 na kujiunga na THT.



Hata hivyo mwaka uliofuata ilimalazimu arudi shule na alilkua akiimba kwenye matamasha mbalimbali ya shule. Lakini ni shindano la Nyuki Live ndilo lililoanza kumng’arisha baada ya kuibuka miongoni mwa washindi kumi akiwa na akina Linnah, Stereo na wengine na kupata recording deal kwa Man Water kutengeneza wimbo wake wa kwanza ulioitwa “Shining Star” aliofanya na Ne-Mo. 


Hata hivyo haukutamba sana. Hio ilikua ni April 2010 baada tu ya kumaliza kidato cha sita. May, alikutana na Duke na kumpa nafasi ya kufanya kiitikio kwenye wimbo wa Nicki Mbishi “Playboy” ikiwa ni kama kumfanyia majaribio ili amsainishe kabisa kufanya naye kazi. Baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo huo, aitengeneza wimbo wake mwenyewe wa ‘Pata raha” ambao ndani yake kulikuwa na watu kama Nicki Mbishi, One na Stereo na kisha kupewa mkataba na dili la kurekodi album nzima M-Lab ambayo ilitoka Februari 14 iitwayo MABOMA ambapo yeye mwenyewe anasema ni neno la kigogo lenye maana ya kutokua karibu na watu wako wa karibu kutokana na utafutaji wa riziki au chochote kile cha neema. 


Album hiyo ina nyimbo kumi nazo ni: Pata Raha Ft. Stereo, One & Nicki Mbishi, Nikikupata, Maumivu, Maumivu (Remix) Ft. One, Naringa Napendwa Ft. Linnah, Samboira, Maboma, Am High Ft. Gosby, Number 1 Fan, na Maneno. Albamu hiyo inapatikana kwa 10,000/=. Pamoja na kumaliza project hiyo na mkataba wake kumalizika, Ben bado anaendelea kufanya kazi na Duke kwani ni muimbaji mmojawapo wa M-Band.

HAMASA NA SAPOTI:
Anasema kapata hamasa kubwa sana kutokana na kuvutiwa na T.I.D kwa hapa Bongo na nje ni John Legend, BabyFace na Maxwell.


Sapoti kubwa sana kutoka kwa mama yake (Sessy) ambapo anasema hakuona uvivu kumpa nauli za kwenda THT na sehemu nyingine za kwenda kufanyia mihangaiko yake ya kimuziki. Anamshukuru sana kwa hilo. Pia akaelekeza shukrani zake THT, Duke na kwa timu nzima ya M-Lab.



SOKO LA MUZIKI WA BONGO:
Ben anadai kuwa soko la muziki wa bongo bado ni bovu kwani halilipi. Pia anasema wasanii wenyewe wanaishusha thamani yao kutokana na kuridhika na kiasi kidogo cha fedha. Urasimu katika mauzo ya kazi zao pia unachangia kuliua soko la muziki bongo.

MATATIZO YA KIMUZIKI:

Kabla: 
Alikutana na matatizo ya kutokuaminika kiuwezo kwani alizinguliwa kwenye studio kibao kabla ya kufika M-Lab, kama Mj Records, Tongwe Records na Fishcrab. Pia anaelezea jinsi alivyokosa ushirikiano kutoka kwa wasanii mbali mbali waliokua na uwezo kumzidi kidogo hasa alipokua THT. Lakini mwenyewe anasema hana kinyongo wala chuki nao kwani kwa sasa ndo washikaji zake sana tu.

Baada: 
Usumbufu kutoka kwa wasichana hasa wa kimapenzi. Ben anasema watu hao wanamkera sana kwani tayari anae mwenza wake.

MIPANGO:
Kuitambulisha rasmi albamu yake na kufanya ziara mikoani na nje ya nchi ili isikike mbali zaidi. Watu wasubiri ngoma yake nyingine kutoka kwenye album na video mpya pia.

HISIA BAADA YA TUZO:
Furaha sana na kujivunia. Pia aliwashukuru watu wote walifanikisha yeye kutwaa tuzo ile, mashabiki na timu nzima ya M-Lab, maprodyuza wake pia. M-Lab walimfanyia kasherehe wakati anafanya show Zhongua Garden, Ijumaa (1 Aprili) ya kumpongeza.

Huyo ndiye Benard Paul a.k.a Ben Pol. Much Love Brother, endelea kukomaa kwani tunatarajia mambo mengi makubwa na mazuri kutoka kwako.

Timu nzima ya rokBrothers, inakutakia kila la kheri kwenye safari yako ya kimuziki na maisha. Pamoja.

0 comments:

Post a Comment

Page viewers