Subscribe:

Follow Us by Email

Ads 468x60px

October 19, 2012

KIDUKU...Style Ya Nywele, Habari Ya Dunia
Mavazi, yanataka uende na wakati...fashion! Dress to Impress wenyewe wanasema. It is also believed that, fashion will never end because it keeps revolving, nguo za zamani zinakuwa modernized, styled na maisha ya kifashion yanaendelea. Aidha kuna aina ya mavazi ambayo hayapitwi na muda wake, yanamaintain status yake kwa muda mrefu, hivyo kumfanya mtu aonekane on fashion and updated kila kukicha. Salute kwa mnaopendeza kwa kupangilia mavazi yenu!
Sasa tutoke huko kwenye mavazi na tuje kwenye eneo jingine ambalo lamfanya mtu aonekane nadhifu zaidi, ofcourse, the reception! No, you guessed wrong, sizungumzii sura, nazungumzia the head, yeah, the head, the hair...Hair Styles exactly!
Nakumbuka enzi zile za FunkyPunky, akina Fresh Prince(Will Smith, Singer,Actor), Andy Cole, Dwight Yorke, Ian Wright(Football Players), Mike Tyson(Boxer) na wengine kibao huku Mike akiweka na Way, dah! Ilikuwa hujatokelezea kama hujaweka huo mtindo kichwani! Achana na Mapala ya akina Michael Jordan na Shaquille O`neal! Kwa upande wangi niliamini ndo itakuwa the forever lasting hairstyle kwa wanaume na kwamba haitokuja kutokea kama ile!
Lakini ghafla, recently imekuja style iliyokamata zaidi attention ya wakaka hadi wadada, ambayo mie kiukweli nilianza kuiona kwa Mr.T, unamkumbuka wewe? Ikazima, then akaja kuiibua tena jamaa mmoja hivi anaitwa Umit Davala...Turkey World Cup 2002, wakumbuka? Achana na kile kidubwana cha Ronaldo! Since Then, style hii imekuwa ikishika hatamu mpaka hivi leo huku watu mbalimbali maarufu wakikiweka kwa style mbalimbali! Check kile cha Neymar, Cristiano Ronaldo, Ngassa, Okwi, Twite mpaka Ommy Dimpoz.
KIDUKU...ndo common name la style hiyo ya nywele hapa kwetu! Kiduku kimeshika kwa kweli!
Comment On This...

0 comments:

Post a Comment

Page viewers