Subscribe:

Follow Us by Email

Ads 468x60px

August 15, 2012

Fabrice Muamba Aacha Soka!

Mchezaji wa timu ya Bolton Wanderers ya Uingereza, mwenye asili ya DRC, Fabrice Muamba, hatimaye ameamua kuachana na soka kabisa kutokana na tatizo lake la moyo.
Licha ya kufanyiwa upasuaji ambao ungeweza kumuwezesha kurejea tena uwanjani, timu ya madaktari, nchini Ubelgiji wamemshauri kuachana na soka ili kuepuka kuhatarisha maisha yake, uamuzi amabao Muamba kaufikia hivi leo kwa masikitiko sana.
Aidha kabla ya kutangaza rasmi kustaafu soka, Fabrice alitoa shukrani zake kwa mashabiki na wadau wa soka duniani kote kwa dua na maombi yao, lakini hana budi kuitizama afya yake kwanza kwani ndo ktu muhimu zaidi.
Ikumbukwe, Muamba alipata tatizo la mshtuko wa moyo wakati wa mechi dhidi ya Tottenham Hotspur, msimu uliopita.
Kila La Heri Fabrice! Tutakumiss Sana!

0 comments:

Post a Comment

Page viewers