Subscribe:

Ads 468x60px

April 26, 2011

Mwana Fa-Unanijua Unanisikia lyrics




Verse I
Ukiwa fukara kamwe huwezi kuwa kiburi/
askini jeuri ni msemo tu usiuweke kweli akili/
Mwanamme kuwa tajiri ni kama demu kuwa mzuri/
demu wako akiwa kwenye kioo we piga simu tafuta dili/
hela hazilali so ukilala wewe tu/
na zina kasi ya kutengezwa hazikungoji uamke mkuu/
mi na'make money mchana,na'make money usiku/
iwe kwa tai au kwa jeans mi naingiza mkwanja babu/
naingiza mkwanja na jua na na giza totoro/
mwenzangu saa unazibagua mi sina nazo mgogoro/
begi mgongoni na ramani kama mzungu/
kabla hujafika nilipo nshafahamu my next move/
pesa ni rock mi ni roll/wana wa long time ago/
hamuwezi kutuachanisha waliojaribu wote wame'fall/
mikuki imepotea farasi wanarudi wenyewe/
waliowapanda wakati wa kwenda wanaomba wafufuliwe/

Choras
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine/
UNANIJUA UNANISKIA?*2/
Punchlines zinafuatana/
UNANIJUA UNANISKIA?*
Punchlines zinaongozana/
UNANIJUA UNANISKIA?/
Punchlines zimegandana/
UNANIJUA UNANISKIA?
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma

Verse II
Inakera,kujua majibu na watu hawaulizi kitu/
we unajua si hatujui ila kaa navyo viote kutu/
Maisha ni kama ubao ila hayaandikwi kwa chaki/
siwezi kupa silaha zote nikikupa kwangu zimebaki/
mi ni limited edition nna mission kabla ya kudanja/
ya kwanza kuwa na mkwanja na ya pili kuwa na mkwanja/
namuweka Mungu kwanza dunia inashindwa nivunja/
nusu haramu nusu halali upande Sheikh na upande Ninja/
Kila bosi ana bosi wake,kama mnyonge na mnyonge wake/
Mola alikupa punje na punje kawapa wengine/
hakutaka unyanyaswe wala unyanyase watu wake/
alichokupa mi hakunipa ni vyetu tutumie sote/
Ukipata nusu ina maana umekosa nusu/
na tuseme anayo Mpoki au Masanja we haikuhusu/
Ni siku ya kwanza ya maisha yangu yaliyobaki/
Hivi ndio nnavyotaka iende huu wimbo ni manuscript/

Choras
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine/
UNANIJUA UNANISKIA?*2/
Punchlines zinafuatana/
UNANIJUA UNANISKIA?*
Punchlines zinaongozana/
UNANIJUA UNANISKIA?/
Punchlines zimegandana/
UNANIJUA UNANISKIA?
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma

Verse III
Sina mjadala na ujinga,sina nafasi ya kuuweka/
umri unasonga sina muda mvi zinasogea zitafika/
sipunguziki mimi ka bei za supermarket/
tuna uzito tofauti kama wa shuka na blanket/
naisafisha sabuni ndio inisafishe maungoni/
so usininyooshee kidole we ni mchafu zaidi ya mimi/
wenzako hawaombi wanashukuru wanapenda walichopata/
omba samaki upewe nyoka,omba upewe usichotaka/

Choras
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine/
UNANIJUA UNANISKIA?*2/
Punchlines zinafuatana/
UNANIJUA UNANISKIA?*
Punchlines zinaongozana/
UNANIJUA UNANISKIA?/
Punchlines zimegandana/
UNANIJUA UNANISKIA?
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma

Yeah
Tumekubaliana kwamba inaisha hivi hivi leo,
haina outro haina nini,
it's yo boy 007 James Bond,
na Hermy B,ofcoz,it's that boy MwanaFA,
The Mastermind himself,B Hits...
We out Yo..Peace...

April 21, 2011

Godzilla-Kingzilla lyrics



INTRO
nigger dont be mad man, its classic

VERSE 1
success zimekuja kwa potential , mi ni boss still naishi ghetto
am soo hood, bado na sell kush ,mi ni hustler man, kila ride mi leo napush
nabadilika  sana cause am the best, walifikiri nimekufa baada ya accident
kila ninachopata weka kwenye memory, baada ya miaka 10 i can write history
niko deep sana kwenye mentally, wanaombea hata nipate supplimentary
now take a glass make a toss, (now whip ur hair back and forth  2)
man macochali, mama zilla i appreciate, mmeniambia no tungi no ciggaret
get off ma way nasikiliza kwenye ride, natoka zangu town naelekea west side

CHORUS
jinsi nilivyo watu wanakaa, king zilla zilla ni balaa
every body knows zilla ni balaa, kwenye game ye ni big change  2

VERSE 2
baada ya kudondosha swaga now the game is mine, wanashangaa kuona kwamba life is on the line
nadondosha style kama buster flip mode, kila baada ya dakika 3 new dresscode
nacheka kwa dharau life is simple, napiga deal na wachina portorico
nachange gear morogoro 1 hr, kwasababu right now nigger i got power
collable za kutosha napiga nonstop, see a made it man now am on top
flow ziko deep kutoka kwenye blood, na huwezi kunizuia its really really hard
nigger i keep it gangstar hard to the core, ur brains nablow with ma fow fow
flow ziki tight zina sound nicely, ladies wanasema zilla we love ur voice

BRIDGE
mi ni gangster ninja, i told ya, am general salutly soldier 4

April 08, 2011

rokPoetry vol.2

What Is A Friend....?

You ask me what a friend is....
Someone who understands
and love you best,
when you are pressed
and need a helping hand.
  
     Someone who gives you courage
     when life is hard to bare,
     though others may forsake you
     a friend is always there.

Someone who sees your sorrow
and read into your heart,
and without a word of question
does more than just his part.

      You ask me a friend is.....
      well, someone tried and true
      who loves to live,
      and lives to give
      the best he/she has to you

Diana
News Department
rokBrothers, 2011

The Handbag/Purse

Here we go again ladies...what do you carry in your Handbag/Purse!?

1. Lip Balm :
Isiwe yoyote tu, iendane na ngozi yako pia iwe ambayo inasaidia katika kuhakikisha lips hazikauki.

2. Lip Stick :
Iendane na ngozi na rangi ya mavazi yako.

3. Angel Face

4. Make Up Kit :
Mara nyingi huwa zina namba mbalimbali zinazowakilisha aina mbalimbali za ngozi.
Hivyo mtu hutakiwa kufahamu aina ya ngozi yake inawakilishwa na namba gani ili aweze kutumia . Husaidia kuiweka ngozi katika hali ya ukavu usio na mafuta.

5. Perfume:
Husaidia kumfanya mtu kutoa harufu nzuri na kuondoa harufu ya jasho ambayo huweza kutoka , kutokana na shughuli mbalimbali za kila siku.

6.Moistured Wipes:
Husaidia kujifutia jasho na mchuruziko wa manukato.

April 04, 2011

Fashion Tips: Casuality


Kama kawaida ya kipande hiki kuzungumzia ubunifu na mitindo ikizingatia nyakati za usasa zaidi ili kukufahamisha ni aina gani ya mtindo unaokwenda na wakati uliopo unaoweza kukutoa chicha mbaya.

Leo tunachungulia Casual Wear, mavazi ya kitanashati ambayo yananata  na kila aina ya mwili halikadhalika yanatambulika kwenye maeneo na nyakati tofauti.

Casuality  ni muonekano ambao miaka yote umekuwa haupitwi na wakati kwani ulikuwepo tokea zamani na mpaka leo hii upo. Ni uvaaji wa mavazi ''Simple'' kama T-Shirts na Jeans au Suruali safi ya kitambaa na viatu flani hivi visivyokua na makuu au mbwembwe nyingi. Wapo pia wanaotupia Shati safi la kitenge, suruali yake ya kawaida tu na relaxive sandals, makobazi. Na je, mtu anapopigilia Shati, Suruali na moka pale chini? Ah, utanashati ulioje.

Nadhani kuna watu bado hajafahamu kuwa Casual Wear ni mavazi fulani ambayo yanaweza kuusitiri mwili wako vizuri na kuonekana nadhifu mbele za watu. Mavazi haya hukubalika Ofisini, kitaani, harusini sometimes hadi kiwenye night clubs na huwa yanampendezesha mwanaume kwa mwanamke.

rokBrothers, 2011

Meza Moja na Ben Pol......



rokBrothers safari hii ilitia maguu hadi katika studio za M-Lab, Kinondoni kwenda kukutana na kufanya mahojiano na Mshindi wa tuzo ya Kili ya Wimbo Bora wa R&B, Ben Pol na kufunguka nae kama hivi:

HISTORIA FUPI:
Wengi tunamfahamu kama Ben Pol lakini jina lake la vitambulisho na vyeti ni Bernard Paul. Ni mtoto wa Pili kwenye familia ya watoto wanne lakini kwa bahati mbaya kaka yake alifariki hivyo kubakia watatu. Baba yake ni mzaliwa na Dodoma na mama yake ni mzaliwa wa Shinyanga. Bernard Paul ni Mgogo halisia.

ELIMU:
Alianza elimu yake ya msingi mwaka 1997 na kumaliza mwaka 2003 katika shule ya msingi Vingunguti. Mwaka 2004 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Dar-Es-Salaam sekondari na kumaliza kidato cha nne mwaka 2007, Novemba. May 2008 aliendelea na elimu yake ya juu katika shule ya sekondari Azania hadi mwaka 2010 alipomaliza kidato cha sita. Baada ya hapo hakuendelea tena na elimu yake ya chuo baada ya kuamua kujiingiza kwenye shughuli za muziki.

MUZIKI:
Ben anasema alipenda kuimba tangu shule ya msingi kwa kuimba nyimbo za watu na kukariri nyimbo zao lakini hadi kufikia kidato cha tatu mwaka 2006 alinza kujifunza kuimba nyimbo zake mwenyewe lakini kutokana na kutingwa na masomo alisubiri hadi alipomaliza kidato cha nne mwaka 2007 na kujiunga na THT.



Hata hivyo mwaka uliofuata ilimalazimu arudi shule na alilkua akiimba kwenye matamasha mbalimbali ya shule. Lakini ni shindano la Nyuki Live ndilo lililoanza kumng’arisha baada ya kuibuka miongoni mwa washindi kumi akiwa na akina Linnah, Stereo na wengine na kupata recording deal kwa Man Water kutengeneza wimbo wake wa kwanza ulioitwa “Shining Star” aliofanya na Ne-Mo. 


Hata hivyo haukutamba sana. Hio ilikua ni April 2010 baada tu ya kumaliza kidato cha sita. May, alikutana na Duke na kumpa nafasi ya kufanya kiitikio kwenye wimbo wa Nicki Mbishi “Playboy” ikiwa ni kama kumfanyia majaribio ili amsainishe kabisa kufanya naye kazi. Baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo huo, aitengeneza wimbo wake mwenyewe wa ‘Pata raha” ambao ndani yake kulikuwa na watu kama Nicki Mbishi, One na Stereo na kisha kupewa mkataba na dili la kurekodi album nzima M-Lab ambayo ilitoka Februari 14 iitwayo MABOMA ambapo yeye mwenyewe anasema ni neno la kigogo lenye maana ya kutokua karibu na watu wako wa karibu kutokana na utafutaji wa riziki au chochote kile cha neema. 


Album hiyo ina nyimbo kumi nazo ni: Pata Raha Ft. Stereo, One & Nicki Mbishi, Nikikupata, Maumivu, Maumivu (Remix) Ft. One, Naringa Napendwa Ft. Linnah, Samboira, Maboma, Am High Ft. Gosby, Number 1 Fan, na Maneno. Albamu hiyo inapatikana kwa 10,000/=. Pamoja na kumaliza project hiyo na mkataba wake kumalizika, Ben bado anaendelea kufanya kazi na Duke kwani ni muimbaji mmojawapo wa M-Band.

HAMASA NA SAPOTI:
Anasema kapata hamasa kubwa sana kutokana na kuvutiwa na T.I.D kwa hapa Bongo na nje ni John Legend, BabyFace na Maxwell.


Sapoti kubwa sana kutoka kwa mama yake (Sessy) ambapo anasema hakuona uvivu kumpa nauli za kwenda THT na sehemu nyingine za kwenda kufanyia mihangaiko yake ya kimuziki. Anamshukuru sana kwa hilo. Pia akaelekeza shukrani zake THT, Duke na kwa timu nzima ya M-Lab.



SOKO LA MUZIKI WA BONGO:
Ben anadai kuwa soko la muziki wa bongo bado ni bovu kwani halilipi. Pia anasema wasanii wenyewe wanaishusha thamani yao kutokana na kuridhika na kiasi kidogo cha fedha. Urasimu katika mauzo ya kazi zao pia unachangia kuliua soko la muziki bongo.

MATATIZO YA KIMUZIKI:

Kabla: 
Alikutana na matatizo ya kutokuaminika kiuwezo kwani alizinguliwa kwenye studio kibao kabla ya kufika M-Lab, kama Mj Records, Tongwe Records na Fishcrab. Pia anaelezea jinsi alivyokosa ushirikiano kutoka kwa wasanii mbali mbali waliokua na uwezo kumzidi kidogo hasa alipokua THT. Lakini mwenyewe anasema hana kinyongo wala chuki nao kwani kwa sasa ndo washikaji zake sana tu.

Baada: 
Usumbufu kutoka kwa wasichana hasa wa kimapenzi. Ben anasema watu hao wanamkera sana kwani tayari anae mwenza wake.

MIPANGO:
Kuitambulisha rasmi albamu yake na kufanya ziara mikoani na nje ya nchi ili isikike mbali zaidi. Watu wasubiri ngoma yake nyingine kutoka kwenye album na video mpya pia.

HISIA BAADA YA TUZO:
Furaha sana na kujivunia. Pia aliwashukuru watu wote walifanikisha yeye kutwaa tuzo ile, mashabiki na timu nzima ya M-Lab, maprodyuza wake pia. M-Lab walimfanyia kasherehe wakati anafanya show Zhongua Garden, Ijumaa (1 Aprili) ya kumpongeza.

Huyo ndiye Benard Paul a.k.a Ben Pol. Much Love Brother, endelea kukomaa kwani tunatarajia mambo mengi makubwa na mazuri kutoka kwako.

Timu nzima ya rokBrothers, inakutakia kila la kheri kwenye safari yako ya kimuziki na maisha. Pamoja.

April 03, 2011

Beauty, Fashion & Trends

Five Must-Have Fashion Accessories: 

     Footwear:  
     Heels, Wedge heels, Sandals depending on the comfortability and trends



     Bags:
     Designer Handbags and bags. A fashion-ate bag/handbag, clutches (shoulder bags). Should be not only  stylish but functional too.

        
            Jewelry: 
     Includes necklaces, bracelets, earings, rings, foot-bracelets and bangles. Go for jewelry that matches the trends as well as that suits your personality.

     
     Hats and Scarves: 
     Depending on seasons (warm or cool).

      
      Sunglasses: 
     Depending on trends, your personal preferences, shape e.t.c. Better stick to the standard ones i.e Black or/and Brown shades but with different frame colours e.g navy blue and Khaki. You can also go for other colours to match your different outfits.
          
Beauty, Fashion & Trends Department
rokBrothers, 2011.

rokPoetry

The Rose That Will Never Die
A rose that will never loose its petals, because I bloom all year long.
I am the rose in your Garden. I am the rose that will wither, why, because “I am God”. 
My love shine in your life and my glory is a sweet, sweet spirit in all rounds.

My spirit begin peace, love, hope, joy and happiness. 
I am the rose that you pick when you buy flower.

By Diana
News Department,
rokBrothers,2011.


Amani na Upendo
Upendo na amani ni nguzo kubwa duniani, unapokuwa navyo unapata furaha moyoni. Kwanza uanepusha shari, zenye kuleta hatari, sababu umejaa upendo, basi vitakupitia mbali. Utaepukana na skendo na za vichochoroni kabali, sababu we ni mtu wa watu kila kitu kitakuwa shwari.

Amini, upendo huongozana na amani, kamwe haviachani  kama historia na hadithi za zamani. Cha muhimu kuzingatia, ili furaha ipate nafasi yenye kusindikizwa na matarumbeta na si milio ya risasi. Anayekukosea msamehe, ajifunze, si kulipiana visasi, hili ni wazo usilipuze, liandike kwenye karatasi likukumbushe,kama kichwani mwako imejaa nafasi. Amani na Upendo, urithi wa pekee wa kizazi hadi vizazi. One Love.

Na Khalifa
News Department
rokBrothers,2011.

Honeysuckle, Pantone's colour of the year

For the past couple of years, Apartment Therapy has eagerly awaited word on Pantone's pick for "color of the year" so we could announce it to all of you. This time, we had a little advance notice, making it easy to share the news right away — so without further ado, the color of the year for 2011 is....HONEYSUCKLE. Honeysuckle is an exceptional vibrant red-based pink shade.

Beauty, Fashion & Trends Department
rokBrothers,2011.

Page viewers