Subscribe:

Ads 468x60px

April 04, 2011

Fashion Tips: Casuality


Kama kawaida ya kipande hiki kuzungumzia ubunifu na mitindo ikizingatia nyakati za usasa zaidi ili kukufahamisha ni aina gani ya mtindo unaokwenda na wakati uliopo unaoweza kukutoa chicha mbaya.

Leo tunachungulia Casual Wear, mavazi ya kitanashati ambayo yananata  na kila aina ya mwili halikadhalika yanatambulika kwenye maeneo na nyakati tofauti.

Casuality  ni muonekano ambao miaka yote umekuwa haupitwi na wakati kwani ulikuwepo tokea zamani na mpaka leo hii upo. Ni uvaaji wa mavazi ''Simple'' kama T-Shirts na Jeans au Suruali safi ya kitambaa na viatu flani hivi visivyokua na makuu au mbwembwe nyingi. Wapo pia wanaotupia Shati safi la kitenge, suruali yake ya kawaida tu na relaxive sandals, makobazi. Na je, mtu anapopigilia Shati, Suruali na moka pale chini? Ah, utanashati ulioje.

Nadhani kuna watu bado hajafahamu kuwa Casual Wear ni mavazi fulani ambayo yanaweza kuusitiri mwili wako vizuri na kuonekana nadhifu mbele za watu. Mavazi haya hukubalika Ofisini, kitaani, harusini sometimes hadi kiwenye night clubs na huwa yanampendezesha mwanaume kwa mwanamke.

rokBrothers, 2011

0 comments:

Post a Comment

Page viewers