Verse I
Ukiwa fukara kamwe huwezi kuwa kiburi/
askini jeuri ni msemo tu usiuweke kweli akili/
Mwanamme kuwa tajiri ni kama demu kuwa mzuri/
demu wako akiwa kwenye kioo we piga simu tafuta dili/
hela hazilali so ukilala wewe tu/
na zina kasi ya kutengezwa hazikungoji uamke mkuu/
mi na'make money mchana,na'make money usiku/
iwe kwa tai au kwa jeans mi naingiza mkwanja babu/
naingiza mkwanja na jua na na giza totoro/
mwenzangu saa unazibagua mi sina nazo mgogoro/
begi mgongoni na ramani kama mzungu/
kabla hujafika nilipo nshafahamu my next move/
pesa ni rock mi ni roll/wana wa long time ago/
hamuwezi kutuachanisha waliojaribu wote wame'fall/
mikuki imepotea farasi wanarudi wenyewe/
waliowapanda wakati wa kwenda wanaomba wafufuliwe/
Choras
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine/
UNANIJUA UNANISKIA?*2/
Punchlines zinafuatana/
UNANIJUA UNANISKIA?*
Punchlines zinaongozana/
UNANIJUA UNANISKIA?/
Punchlines zimegandana/
UNANIJUA UNANISKIA?
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma
Verse II
Inakera,kujua majibu na watu hawaulizi kitu/
we unajua si hatujui ila kaa navyo viote kutu/
Maisha ni kama ubao ila hayaandikwi kwa chaki/
siwezi kupa silaha zote nikikupa kwangu zimebaki/
mi ni limited edition nna mission kabla ya kudanja/
ya kwanza kuwa na mkwanja na ya pili kuwa na mkwanja/
namuweka Mungu kwanza dunia inashindwa nivunja/
nusu haramu nusu halali upande Sheikh na upande Ninja/
Kila bosi ana bosi wake,kama mnyonge na mnyonge wake/
Mola alikupa punje na punje kawapa wengine/
hakutaka unyanyaswe wala unyanyase watu wake/
alichokupa mi hakunipa ni vyetu tutumie sote/
Ukipata nusu ina maana umekosa nusu/
na tuseme anayo Mpoki au Masanja we haikuhusu/
Ni siku ya kwanza ya maisha yangu yaliyobaki/
Hivi ndio nnavyotaka iende huu wimbo ni manuscript/
Choras
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine/
UNANIJUA UNANISKIA?*2/
Punchlines zinafuatana/
UNANIJUA UNANISKIA?*
Punchlines zinaongozana/
UNANIJUA UNANISKIA?/
Punchlines zimegandana/
UNANIJUA UNANISKIA?
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma
Verse III
Sina mjadala na ujinga,sina nafasi ya kuuweka/
umri unasonga sina muda mvi zinasogea zitafika/
sipunguziki mimi ka bei za supermarket/
tuna uzito tofauti kama wa shuka na blanket/
naisafisha sabuni ndio inisafishe maungoni/
so usininyooshee kidole we ni mchafu zaidi ya mimi/
wenzako hawaombi wanashukuru wanapenda walichopata/
omba samaki upewe nyoka,omba upewe usichotaka/
Choras
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine/
UNANIJUA UNANISKIA?*2/
Punchlines zinafuatana/
UNANIJUA UNANISKIA?*
Punchlines zinaongozana/
UNANIJUA UNANISKIA?/
Punchlines zimegandana/
UNANIJUA UNANISKIA?
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma
Yeah
Tumekubaliana kwamba inaisha hivi hivi leo,
haina outro haina nini,
it's yo boy 007 James Bond,
na Hermy B,ofcoz,it's that boy MwanaFA,
The Mastermind himself,B Hits...
We out Yo..Peace...
0 comments:
Post a Comment