Subscribe:

Ads 468x60px

March 25, 2011

Mustafa Hassanali's Harusi Trade Fair

VISIT harusi Trade fair...Tanzania ONE & ONLY annual wedding from 1-3 APRIL from 10AM to 8 PM at Diamond Jubillee Hall.

Visit all the Wedding related Vendors in Tanzania under ONE ROOF , including those from Zanzibar and Arusha

THE WEDDING FASHION SHOW on 2 April from 8 Pm at Diamond Jubilee....

SEE YOU SOON
VISIT : www.harusitradefair.com
email: info@harusitradefair.com

March 17, 2011

Quick talk na Inno,Kanye West.


Ukimuita Inno, Kanye West ataitika bila kusita, ila jina lake la kisheria kabisa na hata kwenye vitambulisho vyake ni Innocent Rwegoshora Mujwahuki. Hata nalo pia ukimuita atakuitikia bila shaka.

Inno, ni miongoni mwa watayarishaji wa muziki hapa Tanzania anayekuja kwa kasi sana akiwa kwenye studios za M-Lab maeneo ya Kinondoni, Dar-es-salaam. Akizungumzia maisha yake ya kimuziki, anasema kuwa yeye amezaliwa na kuukuta muziki kwenye familia yake,kwani Marehemu baba yake alikuwa ni mpiga kinanda kanisani. Akiwa bado mdogo, baba yake alikuwa akimfundisha jinsi na kupiga kinanda na kumsimamia na ndipo na yeye akaanza kuvutiwa na fani hiyo.
Baba yake alifariki dunia mwaka 2005 wakati yupo kidato cha nne.

"Baada ya baba kufariki na mimi kumaliza kidato cha nne, nikawa nipo zangu tu nyumbani nachezea kinanda nikicopy nyimbo za nje huku nikijiimbia mwenyewe, ndipo siku moja mama yangu alinifuata na kunitania kwamba mbona siufanyi huo muziki sehemu yoyote ile; sio kanisani sio mitaani, basi angalau nifanye bongo flavour nieleweke, nami  nikaipokea kiutani hivyohivyo lakini nikaja kugundua kuwa alikuwa na wazo zuri sana." alisema Inno.
.
Alipoanza kusikia kuhusu THT (Tanzania House of Talents) ndipo alipouona mwanga wa yeye kuweza kufanya muziki kwana alikuwa akiishi maeneo ya Manyanya kipindi hicho na THT iko mitaa ya Moroco, ndipo siku moja akajikuta yupo kwenye kituo cha THT na kukutana uso kwa uso na Barnaba ndani ya THT na kuuanza kuzungumza nae kuusu uwezekano wa yeye kujiunga kama mpiga vyombo, akelekezwa kwa jamaa mmoja anaitwa Hamza. Baada ya kukutanishwa na mpiga kinanda mwingine,Mosse pamoja na mpiga vyombo na muziki wa asili Musa Vipajivingi, ndipo nuru ya Inno ilipowaka.

Musa alikuwa ni mpiga kinanda aliyekuwa na taaluma ya utayarishaji wa muziki pia (M-Lab) na ndiye yeye ambaye alimfungulia milango Inno kujiunga na M-Lab kwani alikuwa akitamani kufanya utayarishaji wa muziki studioni.Na 'package' iliyoletwa M-Lab kutoka THT kama "Robo Saa" ya Amini, "Atatamani" ya Linah, "Wapo" ya Ditto (ilifanyika Ngoma Records kwa Tuddy Thomas) na "Wrong Number" ya Barnaba na Linah ndo zilizonza kumtambulisha rasmi Inno kwenye ulimwengu wa 'music production' kwani alizisimamia vilivyo na kuzifanya zitikise chati na stesheni mbalimbali (Kipindi hicho hakuwa M-Lab rasmi). Mwaka 2010 alijiunga rasmi na M-Lab.

Inno (Kanye), hana project yoyote hivi sasa, kwani aliokua nayo ni kutengeneza albamu ya Ben Pol ambayo ameshaikamilisha na 70% ya albamu nzima kaifanya yeye akishirikiana na Duke, ikiwemo ngoma ya "Nikikupata". Zaidi kinachomuweka 'busy' hivi sasa ni kujishughulisha sana na M-Band.

Akizungumzia suala la nani aliyemvutia na kumshawishi kuingia kwenye maswala ya musiki alisema "Kwanza ni wazazi wangu, nawashukuru sana na pili ni Duke Tachez, ambaye kiukweli kabla sijaanza kuamua kufanya production nilikua navutiwa sana naye, na nimejikuta nashindwa kutoka kwenye elements zake kuanzia midundo na kila kitu yani nafeel sana kufanya Hip-Hop pia. Lakini kwa upande wa nje ni Timbaland na Kanye West."

Aidha Inno pia alizungumzia suala la soko la muziki wa bongo na kudai kuwa limeshikiliwa sana na vyombo vya habari. Yani mtu anashindwa kufanya kitu, akihofia vyombo vya habari vitaandikaje. Kwamba sasa mtu anafanya kazi kufuata vyombo vya habari na si matakwa yake. Ni suala baya sana ambalo yeye anadhani linachochea kuua au litaua kabisa soko la muziki Tanzania.

"Ukiachana na hayo, kiukweli bado sijaanza kuzipata changamoto za kimuziki au matatizo kwani bado nalelewa na M-Lab." aliendelea kuongezea Inno.

Kwa mipango yake ya baadae, anadai kuwa anataka kurudi shule kwani hakumaliza kutokana na matatizo ya ada, hivyo anajipanga zaidi kifedha ili arudi kusomea, Socioliogy au Human Resources na kwa upande wa muziki anatamani kuwa na studio yake mwenyewe.

Innocent, alimaliza shule ya msingi Kibasila mwaka 2000 na kuendelea na masomo yake ya sekondari kuanzia mwaka 2001 kwenye shule ya Lwandai iliyopo Lushoto, lakini alipofika kidato cha 3 mwaka 2003, akahamia St.Anne Marie na ndipo alipomalizia elimu yake ya sekondari mwaka 2005. Akaendelea na elimu yake ya juu Bagamoyo alipokuwa akichukua mchepuo wa HGL na kumaliza kidato cha sita mwaka 2008. Akajiunga na chuo cha Tumaini ambapo alikuwa akisomea Mass Communication & Public Relation mpaka alipokuja kuacha mwaka jana (2010) kwa matatizo ya ada.

Huyo ndio, Innocent, fupisha muite Inno a.k.a Kanye West wa pande za Gongo La Mboto, ambaye kwa sasa ameshatengeneza ngoma kadhaa tangu ajiunge M-Lab yeye kama yeye, kama "Pretty" ya G5 ft. Ben Pol na "Nipe nafasi" ya Muba.

Amani kwako kaka na kila la kheri kwenye malengo yako na kazi zako. "Like Father, Like Son" ndivyo wasemavyo wenzetu! Pamoja sana!

rokBrothers, Salute you bro.

March 10, 2011

Meza moja na Peres Paul


Ukishuka Sinza Mori kisha ukaifuata njia ya kuelekea hoteli ya Johannesburg utakutana na ofisi za TAMWA ambazo zipo sambamba na kanisa la Word Alive. Fanya kama unaingia mle kanisani utakutana uso kwa uso na Video studios ziitwaazo Matrix Inc. mali halali ya Peres Paul ambaye pia ndiye director.

Matrix Inc. ni studio za kutengenezea videos hasa video za muziki iliyoanzishwa mnamo mwaka 2009. Akiizungumzia studio hiyo Peres alisema kuwa studio hiyo ni mali yake mwenyewe lakini akipata sapoti ya nguvu kutoka kwa familia na hasa kaka yake Baraka Paul

Peres akielezea baadhi ya project alizo nazo anasema PNC-Shino ni miongoni mwa wasanii ambao anafany nao kazi na alianza kuwa na project naye kuanzia mwishoni mwa mwaka 2009 kuja 2010 na ameshafanya naye kazi kadha wa kadha zikiwemo "Kipenzi" aliyomshirikisha Nemo, "Kwanini" aliyofanya na Bushoke na video mpya kabisa ya PNC inayofanya vyema kwenye stesheni za video ya "Tuzungumze" iliyotoka mwezi Februari mwaka huu. 

Aidha kazi nyingine aliyoitoa hivi karibuni ni ya Imam Kibe akiwashirikisha Chege na Godzilla iitwayo "Sihitaji Kupenda" iliyotoka Januari. Kazi zingine alizofanya na kuvuma ni pamoja na "Matatizo" ya J.I, "Mkali Wao" ya Stolo na Qjay, "Uzoefu" ya Salu T, "Imekula Kwangu" ya Dr.Kumpeneka, "Wanichoma" ya Jai na Blad Key, "Darasa Huru" ya Imam Kibe, Toleo lakwanza la "Ni wewe"ya Nay ambayo kwa sasa yaitwa "Hello".

Kwa sasa, anamalizia kutengeneza video ya One Incredible iitwayo "Pure Number" ambapo kwa mujibu wa Peres, inatarajiwa kuwa hewani hivi karibuni hivyo wapenzi wa Hip-Hop wakae tayari kuipoke ngoma hii tamu ilisukwa vilivyo na director huyu ambaye huitaji Kilo 5(Laki Tano) yako tu kukufanikiashia kazi yako.

Peres pia anasema kuna baadhi ya kadhi ambazo huwa anafanya na mtayarishaji wa Muziki, Duke wa M-Lab na kusema kuwa huzibaatiza kwa jina la "The Definition Pictures" na mfano wa kazi hizo ni "Uzoefu" ya Salu T na "Pure Number" ya One Incredible.

Akizungumzia maisha yake ya kimuziki, anasema kuwa yeye hajawahi kusomea jinsi ya kutengeneza video bali ni utundu wake mwenyewe tu. Peres Alisoma shule ya sekondari Musoma kabla ya kusomea computer maintanance UCC.

Kwenye soko la video, alisema kuwa inalipa kimtindo sema kikwazo kikubwa ni majungu ambayo maproducer wenyewe kwa wenyewe hufanyiana. Kitu ambacho amekilaani sana.

Kwa sasa Peres anatazamia kuingia kwenye tasnia ya kutengeneza movie na bado anachukua kozi kupitia mtandaoni (Internet).

Big Up kwako kaka na Kila la heri kwenye kazi zako zote zinazofuata. One Love.
rokBrothers, Salute you.

March 06, 2011

Fashion tips: So in for the Ladies.

Well kwenye session hii unapata kufahamu ni mavazi gani au style gani ya mavazi, nywele na viatu vinyoendana na wakati uliopo. Leo tunaona ni jinsi gani mwanamke anayependa kwenda na wakati anavyopendeza akivaa Shorts, over a tight skin jeans na a body fit blouse! Na kupendezesha zaidi, ni pale anapotupia scarf inayoendana(match) with the outfits with fancy high heeled shoes. Thats what so in ladies............tupia tuoneeee!

March 05, 2011

Meza moja na Duke Tachez.




Duke “Duke Tachez” Gervalius ni jina ambalo linaweza likawa geni kwa wachache sana, ila kwa walio wengi huweza kumfahamu kwa sababu ya ufuatiliaji na mapenzi ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.


Kwa kifupi , Duke ni mtayarishaji ama Producer wa muziki huu wa kizazi kipya akifanya kazi kwenye recording label ya Music Lab (M.Lab) iliyopo maeneo ya kinondoni, Dar-es-salaam. 

Akielezea historia yake ya muziki, Duke, anasema alianza kujishughulisha na muziki mwaka 1997 akiwa kama EMCEE ndani ya kundi la la SEWA SIDE, kabla ya kuanza kujifunza Udj chini ya Dj PQ ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa watu wanaounda kundi hilo, hiyo ilikuwa ni mwaka 1999. 

Mwaka 2001, alifanikiwa kurekodi wimbo wa kwanza akiwa kama EMCEE kwenye kundi ulioitwa 'WINGU LA MASHAKA' iliyotayarishwa na Proffessor Ludigo ndani ya MJ Records na ngoma nyingine iliyoitwa “Ujumbe Na Maswali” ilipikwa na Solomon Lamba ndani ya studio za Emptysoulz. Kwa bahati mbaya ngoma zote mbili hazikupata airtime ya kutosha. Kutokana na ugumu wa kurekodi wimbo na kundi la SEWA SIDE kutokuwa serious sana na record deal walioipata ndani ya Emptysoulz, alijikuta anaacha hadi kuandika na kuja kuwa na fikra kwamba hata yeye mwenyewe anaweza kuproduce muziki.

Alipokuwa Emptysoulz alijifunza kupiga kinanda kidogo ndipo alipoamua kutafuta na applications za softwares on beats, kwasababu alikuwa na kompyuta nyumbani kwao, ndipo alipokutana na Partrick Gondwe, aliyemsaidia baadhi ya softwares ikiwemo fruity loops ambayo aliwahi kuijaribu akiwa Emptysoulz, na ndipo alipoanza kunyonga beats mwenyewe kutokana na kuupenda na kuvutiwa na midundo ya Hip-Hop.

Kabla ya kufikia M-Lab, Duke, akiwa kama independent producer ashawahi kufanya kazi ndani ya studio mbalimbali kama; Bongo Records, Kama Kawa Records, Dhahabu Records, Pasu Kwa Pasu, 41 Records, Tongwe Records na nyingine kibao lakini yote ikiwa ni pitapita za kutimiza lengo lake la kuwa na studio yake mwenyewe. Ambapo basi akiwa kama Independently Producer aliweza kutengeneza ngoma kama Zero-Witness, Traveller-Solo Thang, Ripoti za Mtaani-Fid Q na nyingine nyingi kali.

Duke alipokuwa anaelezea projects zake za sasa na baadae alisema kuwa kwa sasa ana project ya launching ya mixtape ya The Element Vol.1 ambayo uzinduzi wake ulishafanyika hapa Dar-es-salaam na mixtape zimesambazwa na kuanza kuuzwa, na ana mipango ya kuizindua mikoani halikadhalika. Aidha alisema kuwa, The Element mixtape ni muendelezo ambao utakua ukitoka kila baada ya MIEZI MIWILI (2) akisema ni iwe changamoto kwa maproducer wengine. Project hii itakuwa inawajumuisha wasanii waliomo ndani ya M-Lab kama One, Stereo, Nikki Mbishi, Grace Matata, Techla, Ben pol na wasanii wengine wengi. 

Mixtape hii ni ya pili kufanya baada ya kutengeneza ya kwanza iliyoitwa Kitaani Vol.1 lakini ilikosa mwendelezo wake. Hata hivyo, Duke, anasema anatarajia kufanya muendelezo wake sometime soon! Pia aliongezea kuizungumzia Element kwamba ni zaidi ya muziki pekee uliomo ndani yake na ndio maana kwenye uzinduzi iliInvolve mambo ya Clothings na Peotry ama ushairi ambazo ni miongoni mwa elements ama nguzo muhimu za Hip-Hop, ambayo ndo music genre anayohusika nayo kwa sana. Hivyo The Element ni utamaduni.

Akizungumzia uhusiano wa M-Lab na M-band, Duke, anasema kuwa zote zipo chini ya mwamvuli mmoja ila zinafanya kazi tofauti. Pia alisistiza kuwa M-Lab ni recording label yenye studio ndani yake ambapo; Patrick Gondwe ni Manager wa studio na pia ni Manager wa wasanii walioko chini ya studio hiyo. Licha ya yeye mwenyewe kuwa producer, pia ni Production Manager ndani ya M.lab na kuwataja maproducer wengine kama Inno, Willy, Den Texas na KG pia kuna composer kama William ambao wote wanashirikiana kutoa ladha tamu kutoka M-Lab. Hits kama Nikikupata, Maumivu na Pata Raha za Ben Pol, zimefanywa na Inno kusaidiana na Duke halikadhalika kwa Willy ambaye katengeneza hits singles za Grace Matata zote ikiwemo Wimbo, Free Soul na Nyakati.

Kwa upande wa Music Industry nchini, Duke alidai kuwa soko la muziki bongo limekufa kutokana na kukosekana kwa credits za kutosha sana sana na kusema kuwa wabongo inabidi wainuke kusapoti wasanii na muziki wao.

Aidha alielezea ujio wa maproducer wapya kila kukicha kama ni kitu cha kufurahisha kwasababu inaleta changamoto mpya na kuchochea maendeleo ya muziki nchini. Kwa sababu, uwepo wa maproducer wachache unazorotesha muziki wa kibongo kutokana msongamano wa nyimbo. Hivyo kwa sasa msanii sio lazima akarekodi ngoma yake kwa Duke pekee, bali anaweza rekodi kwenye studio nyingine na akapata hit kama kawaida. Kwa mantiki hiyo, idadi ya hits kwenye muziki wa kibongo zinazongezeka kila siku ni kitu ambacho ni kizuri sana kwenye soko letu la muziki.

“Ni wakati wa watanzania kutambua na kuuthamini muziki wao kwa kuwasapoti wasanii na kazi zao na kuwakosoa pia pale wanapokosea ili kuleta maendeleo ya muziki nchini” alisisitiza Duke.

Duke alimaliza elimu yake ya sekondari Makongo High School kabla ya kupiga mafunzo ya technology kwenye chuo cha Learn IT na kumaliza mwaka 2003.
rokBrothers, Salut you bro.

March 03, 2011

Fashion Tips

Unapozungumzia fashion, uanaamanisha mtindo uliopo kwa kifupi tu. Yaani mtindo na matendo ambayo yanayovuma kwenye jamii kwa kipindi kilichopo ambapo inaweza kuwa kwenye mavazi na hata viatu. Wengi wanadescribe fashion kama fanciness na kuwa tofauti kidogo.

Kihistoria, asili ya fashion au mitindo ina asili ya Ulaya magharibi kwenye nchi kama Ujerumani, Italia na hata Ufaransa, hasa kwenye kipindi cha karne ya 14 ambapo tunawazungumzia wabunifu wa mavazi kama Marie Antoinette, James Lauver na Fernand Braudel.

Fashion Industry ilianza kushika hatamu kuanzia karne ya 19 na 20 kutokana na mapinduzi ya viwanda na uwepeo wa zana nyingi za ubunifu kama mashine na n.k.


Kwa Tanzania, Mitindo bado haijavuma sana kutokana na kukosekana muamko. Shukrani sana kwa wabunifu maarufu hapa nchini, Ally Remtullah, Mustafa Hassanali na Khadija Mwanamboka katika jitihada zao za kuiweka fashion kwenye ramani ya Tanzania. Stay tuned kwa more fashion news kupitia hapahapa Fashion tips. Coming Soon.

Page viewers