Kwa kifupi , Duke ni mtayarishaji ama Producer wa muziki huu wa kizazi kipya akifanya kazi kwenye recording label ya Music Lab (M.Lab) iliyopo maeneo ya kinondoni, Dar-es-salaam.
Akielezea historia yake ya muziki, Duke, anasema alianza kujishughulisha na muziki mwaka 1997 akiwa kama EMCEE ndani ya kundi la la SEWA SIDE, kabla ya kuanza kujifunza Udj chini ya Dj PQ ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa watu wanaounda kundi hilo, hiyo ilikuwa ni mwaka 1999.
Mwaka 2001, alifanikiwa kurekodi wimbo wa kwanza akiwa kama EMCEE kwenye kundi ulioitwa 'WINGU LA MASHAKA' iliyotayarishwa na Proffessor Ludigo ndani ya MJ Records na ngoma nyingine iliyoitwa “Ujumbe Na Maswali” ilipikwa na Solomon Lamba ndani ya studio za Emptysoulz. Kwa bahati mbaya ngoma zote mbili hazikupata airtime ya kutosha. Kutokana na ugumu wa kurekodi wimbo na kundi la SEWA SIDE kutokuwa serious sana na record deal walioipata ndani ya Emptysoulz, alijikuta anaacha hadi kuandika na kuja kuwa na fikra kwamba hata yeye mwenyewe anaweza kuproduce muziki.
Alipokuwa Emptysoulz alijifunza kupiga kinanda kidogo ndipo alipoamua kutafuta na applications za softwares on beats, kwasababu alikuwa na kompyuta nyumbani kwao, ndipo alipokutana na Partrick Gondwe, aliyemsaidia baadhi ya softwares ikiwemo fruity loops ambayo aliwahi kuijaribu akiwa Emptysoulz, na ndipo alipoanza kunyonga beats mwenyewe kutokana na kuupenda na kuvutiwa na midundo ya Hip-Hop.
Kabla ya kufikia M-Lab, Duke, akiwa kama independent producer ashawahi kufanya kazi ndani ya studio mbalimbali kama; Bongo Records, Kama Kawa Records, Dhahabu Records, Pasu Kwa Pasu, 41 Records, Tongwe Records na nyingine kibao lakini yote ikiwa ni pitapita za kutimiza lengo lake la kuwa na studio yake mwenyewe. Ambapo basi akiwa kama Independently Producer aliweza kutengeneza ngoma kama Zero-Witness, Traveller-Solo Thang, Ripoti za Mtaani-Fid Q na nyingine nyingi kali.
Duke alipokuwa anaelezea projects zake za sasa na baadae alisema kuwa kwa sasa ana project ya launching ya mixtape ya The Element Vol.1 ambayo uzinduzi wake ulishafanyika hapa Dar-es-salaam na mixtape zimesambazwa na kuanza kuuzwa, na ana mipango ya kuizindua mikoani halikadhalika. Aidha alisema kuwa, The Element mixtape ni muendelezo ambao utakua ukitoka kila baada ya MIEZI MIWILI (2) akisema ni iwe changamoto kwa maproducer wengine. Project hii itakuwa inawajumuisha wasanii waliomo ndani ya M-Lab kama One, Stereo, Nikki Mbishi, Grace Matata, Techla, Ben pol na wasanii wengine wengi.
Mixtape hii ni ya pili kufanya baada ya kutengeneza ya kwanza iliyoitwa Kitaani Vol.1 lakini ilikosa mwendelezo wake. Hata hivyo, Duke, anasema anatarajia kufanya muendelezo wake sometime soon! Pia aliongezea kuizungumzia Element kwamba ni zaidi ya muziki pekee uliomo ndani yake na ndio maana kwenye uzinduzi iliInvolve mambo ya Clothings na Peotry ama ushairi ambazo ni miongoni mwa elements ama nguzo muhimu za Hip-Hop, ambayo ndo music genre anayohusika nayo kwa sana. Hivyo The Element ni utamaduni.
Akizungumzia uhusiano wa M-Lab na M-band, Duke, anasema kuwa zote zipo chini ya mwamvuli mmoja ila zinafanya kazi tofauti. Pia alisistiza kuwa M-Lab ni recording label yenye studio ndani yake ambapo; Patrick Gondwe ni Manager wa studio na pia ni Manager wa wasanii walioko chini ya studio hiyo. Licha ya yeye mwenyewe kuwa producer, pia ni Production Manager ndani ya M.lab na kuwataja maproducer wengine kama Inno, Willy, Den Texas na KG pia kuna composer kama William ambao wote wanashirikiana kutoa ladha tamu kutoka M-Lab. Hits kama Nikikupata, Maumivu na Pata Raha za Ben Pol, zimefanywa na Inno kusaidiana na Duke halikadhalika kwa Willy ambaye katengeneza hits singles za Grace Matata zote ikiwemo Wimbo, Free Soul na Nyakati.
Kwa upande wa Music Industry nchini, Duke alidai kuwa soko la muziki bongo limekufa kutokana na kukosekana kwa credits za kutosha sana sana na kusema kuwa wabongo inabidi wainuke kusapoti wasanii na muziki wao.
Aidha alielezea ujio wa maproducer wapya kila kukicha kama ni kitu cha kufurahisha kwasababu inaleta changamoto mpya na kuchochea maendeleo ya muziki nchini. Kwa sababu, uwepo wa maproducer wachache unazorotesha muziki wa kibongo kutokana msongamano wa nyimbo. Hivyo kwa sasa msanii sio lazima akarekodi ngoma yake kwa Duke pekee, bali anaweza rekodi kwenye studio nyingine na akapata hit kama kawaida. Kwa mantiki hiyo, idadi ya hits kwenye muziki wa kibongo zinazongezeka kila siku ni kitu ambacho ni kizuri sana kwenye soko letu la muziki.
“Ni wakati wa watanzania kutambua na kuuthamini muziki wao kwa kuwasapoti wasanii na kazi zao na kuwakosoa pia pale wanapokosea ili kuleta maendeleo ya muziki nchini” alisisitiza Duke.
Duke alimaliza elimu yake ya sekondari Makongo High School kabla ya kupiga mafunzo ya technology kwenye chuo cha Learn IT na kumaliza mwaka 2003.
rokBrothers, Salut you bro.
Noma sana duke touch
ReplyDelete