Ukimuita Inno, Kanye West ataitika bila kusita, ila jina lake la kisheria kabisa na hata kwenye vitambulisho vyake ni Innocent Rwegoshora Mujwahuki. Hata nalo pia ukimuita atakuitikia bila shaka.
Inno, ni miongoni mwa watayarishaji wa muziki hapa Tanzania anayekuja kwa kasi sana akiwa kwenye studios za M-Lab maeneo ya Kinondoni, Dar-es-salaam. Akizungumzia maisha yake ya kimuziki, anasema kuwa yeye amezaliwa na kuukuta muziki kwenye familia yake,kwani Marehemu baba yake alikuwa ni mpiga kinanda kanisani. Akiwa bado mdogo, baba yake alikuwa akimfundisha jinsi na kupiga kinanda na kumsimamia na ndipo na yeye akaanza kuvutiwa na fani hiyo.
Baba yake alifariki dunia mwaka 2005 wakati yupo kidato cha nne.
"Baada ya baba kufariki na mimi kumaliza kidato cha nne, nikawa nipo zangu tu nyumbani nachezea kinanda nikicopy nyimbo za nje huku nikijiimbia mwenyewe, ndipo siku moja mama yangu alinifuata na kunitania kwamba mbona siufanyi huo muziki sehemu yoyote ile; sio kanisani sio mitaani, basi angalau nifanye bongo flavour nieleweke, nami nikaipokea kiutani hivyohivyo lakini nikaja kugundua kuwa alikuwa na wazo zuri sana." alisema Inno.
.
Alipoanza kusikia kuhusu THT (Tanzania House of Talents) ndipo alipouona mwanga wa yeye kuweza kufanya muziki kwana alikuwa akiishi maeneo ya Manyanya kipindi hicho na THT iko mitaa ya Moroco, ndipo siku moja akajikuta yupo kwenye kituo cha THT na kukutana uso kwa uso na Barnaba ndani ya THT na kuuanza kuzungumza nae kuusu uwezekano wa yeye kujiunga kama mpiga vyombo, akelekezwa kwa jamaa mmoja anaitwa Hamza. Baada ya kukutanishwa na mpiga kinanda mwingine,Mosse pamoja na mpiga vyombo na muziki wa asili Musa Vipajivingi, ndipo nuru ya Inno ilipowaka.
Musa alikuwa ni mpiga kinanda aliyekuwa na taaluma ya utayarishaji wa muziki pia (M-Lab) na ndiye yeye ambaye alimfungulia milango Inno kujiunga na M-Lab kwani alikuwa akitamani kufanya utayarishaji wa muziki studioni.Na 'package' iliyoletwa M-Lab kutoka THT kama "Robo Saa" ya Amini, "Atatamani" ya Linah, "Wapo" ya Ditto (ilifanyika Ngoma Records kwa Tuddy Thomas) na "Wrong Number" ya Barnaba na Linah ndo zilizonza kumtambulisha rasmi Inno kwenye ulimwengu wa 'music production' kwani alizisimamia vilivyo na kuzifanya zitikise chati na stesheni mbalimbali (Kipindi hicho hakuwa M-Lab rasmi). Mwaka 2010 alijiunga rasmi na M-Lab.
Inno (Kanye), hana project yoyote hivi sasa, kwani aliokua nayo ni kutengeneza albamu ya Ben Pol ambayo ameshaikamilisha na 70% ya albamu nzima kaifanya yeye akishirikiana na Duke, ikiwemo ngoma ya "Nikikupata". Zaidi kinachomuweka 'busy' hivi sasa ni kujishughulisha sana na M-Band.
Akizungumzia suala la nani aliyemvutia na kumshawishi kuingia kwenye maswala ya musiki alisema "Kwanza ni wazazi wangu, nawashukuru sana na pili ni Duke Tachez, ambaye kiukweli kabla sijaanza kuamua kufanya production nilikua navutiwa sana naye, na nimejikuta nashindwa kutoka kwenye elements zake kuanzia midundo na kila kitu yani nafeel sana kufanya Hip-Hop pia. Lakini kwa upande wa nje ni Timbaland na Kanye West."
Aidha Inno pia alizungumzia suala la soko la muziki wa bongo na kudai kuwa limeshikiliwa sana na vyombo vya habari. Yani mtu anashindwa kufanya kitu, akihofia vyombo vya habari vitaandikaje. Kwamba sasa mtu anafanya kazi kufuata vyombo vya habari na si matakwa yake. Ni suala baya sana ambalo yeye anadhani linachochea kuua au litaua kabisa soko la muziki Tanzania.
"Ukiachana na hayo, kiukweli bado sijaanza kuzipata changamoto za kimuziki au matatizo kwani bado nalelewa na M-Lab." aliendelea kuongezea Inno.
Kwa mipango yake ya baadae, anadai kuwa anataka kurudi shule kwani hakumaliza kutokana na matatizo ya ada, hivyo anajipanga zaidi kifedha ili arudi kusomea, Socioliogy au Human Resources na kwa upande wa muziki anatamani kuwa na studio yake mwenyewe.
Innocent, alimaliza shule ya msingi Kibasila mwaka 2000 na kuendelea na masomo yake ya sekondari kuanzia mwaka 2001 kwenye shule ya Lwandai iliyopo Lushoto, lakini alipofika kidato cha 3 mwaka 2003, akahamia St.Anne Marie na ndipo alipomalizia elimu yake ya sekondari mwaka 2005. Akaendelea na elimu yake ya juu Bagamoyo alipokuwa akichukua mchepuo wa HGL na kumaliza kidato cha sita mwaka 2008. Akajiunga na chuo cha Tumaini ambapo alikuwa akisomea Mass Communication & Public Relation mpaka alipokuja kuacha mwaka jana (2010) kwa matatizo ya ada.
Huyo ndio, Innocent, fupisha muite Inno a.k.a Kanye West wa pande za Gongo La Mboto, ambaye kwa sasa ameshatengeneza ngoma kadhaa tangu ajiunge M-Lab yeye kama yeye, kama "Pretty" ya G5 ft. Ben Pol na "Nipe nafasi" ya Muba.
Amani kwako kaka na kila la kheri kwenye malengo yako na kazi zako. "Like Father, Like Son" ndivyo wasemavyo wenzetu! Pamoja sana!
rokBrothers, Salute you bro.
0 comments:
Post a Comment