Subscribe:

Ads 468x60px

March 10, 2011

Meza moja na Peres Paul


Ukishuka Sinza Mori kisha ukaifuata njia ya kuelekea hoteli ya Johannesburg utakutana na ofisi za TAMWA ambazo zipo sambamba na kanisa la Word Alive. Fanya kama unaingia mle kanisani utakutana uso kwa uso na Video studios ziitwaazo Matrix Inc. mali halali ya Peres Paul ambaye pia ndiye director.

Matrix Inc. ni studio za kutengenezea videos hasa video za muziki iliyoanzishwa mnamo mwaka 2009. Akiizungumzia studio hiyo Peres alisema kuwa studio hiyo ni mali yake mwenyewe lakini akipata sapoti ya nguvu kutoka kwa familia na hasa kaka yake Baraka Paul

Peres akielezea baadhi ya project alizo nazo anasema PNC-Shino ni miongoni mwa wasanii ambao anafany nao kazi na alianza kuwa na project naye kuanzia mwishoni mwa mwaka 2009 kuja 2010 na ameshafanya naye kazi kadha wa kadha zikiwemo "Kipenzi" aliyomshirikisha Nemo, "Kwanini" aliyofanya na Bushoke na video mpya kabisa ya PNC inayofanya vyema kwenye stesheni za video ya "Tuzungumze" iliyotoka mwezi Februari mwaka huu. 

Aidha kazi nyingine aliyoitoa hivi karibuni ni ya Imam Kibe akiwashirikisha Chege na Godzilla iitwayo "Sihitaji Kupenda" iliyotoka Januari. Kazi zingine alizofanya na kuvuma ni pamoja na "Matatizo" ya J.I, "Mkali Wao" ya Stolo na Qjay, "Uzoefu" ya Salu T, "Imekula Kwangu" ya Dr.Kumpeneka, "Wanichoma" ya Jai na Blad Key, "Darasa Huru" ya Imam Kibe, Toleo lakwanza la "Ni wewe"ya Nay ambayo kwa sasa yaitwa "Hello".

Kwa sasa, anamalizia kutengeneza video ya One Incredible iitwayo "Pure Number" ambapo kwa mujibu wa Peres, inatarajiwa kuwa hewani hivi karibuni hivyo wapenzi wa Hip-Hop wakae tayari kuipoke ngoma hii tamu ilisukwa vilivyo na director huyu ambaye huitaji Kilo 5(Laki Tano) yako tu kukufanikiashia kazi yako.

Peres pia anasema kuna baadhi ya kadhi ambazo huwa anafanya na mtayarishaji wa Muziki, Duke wa M-Lab na kusema kuwa huzibaatiza kwa jina la "The Definition Pictures" na mfano wa kazi hizo ni "Uzoefu" ya Salu T na "Pure Number" ya One Incredible.

Akizungumzia maisha yake ya kimuziki, anasema kuwa yeye hajawahi kusomea jinsi ya kutengeneza video bali ni utundu wake mwenyewe tu. Peres Alisoma shule ya sekondari Musoma kabla ya kusomea computer maintanance UCC.

Kwenye soko la video, alisema kuwa inalipa kimtindo sema kikwazo kikubwa ni majungu ambayo maproducer wenyewe kwa wenyewe hufanyiana. Kitu ambacho amekilaani sana.

Kwa sasa Peres anatazamia kuingia kwenye tasnia ya kutengeneza movie na bado anachukua kozi kupitia mtandaoni (Internet).

Big Up kwako kaka na Kila la heri kwenye kazi zako zote zinazofuata. One Love.
rokBrothers, Salute you.

0 comments:

Post a Comment

Page viewers