Subscribe:

Ads 468x60px

July 26, 2012

Mwimbaji The Voice Aliyepata Ajali Aendelea Vizuri

                                                                                                                                                                                                              Mwimbaji wa kundi la muziki wa injili wanandugu, The Voice, Obed Mark aliyepata ajali ya Bajaj hivi karibuni maeneo ya Sinza, Kamanyola, anaendelea vizuri.
Akizungumza kwa njia ya simu jana wakitoka hospitali Kinondoni kuelekea nyumbani, Magomeni-Kagera, mmoja wa wanamuziki wanaounda kundi hilo, Josiah Sadock, aliwashukuru mashabiki na wadau wote waliokuwa wakimuombea mwenzao huyo apone haraka.
"Obed anaendelea vizuri, tunashukuru Mungu na sasa twaelekea nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka na kuandikiwa dawa" Alisema Josiah.
Aidha katika ukurasa wao wa Facebook, leo ThevoiceTZ waliandika kuwa mwenzao anaendelea vizuri hivyo wazidi kumuombea na bila shaka dawa alizopewa zitamsaidia apone haraka na kurudi katika hali yake ya awali.
The Voice, wanatarajiwa kutoa burudani kwenye tamasha la LOVE TANZANIA with Andrew Palau hapo Agosti 11-12.
Uongozi wa rokBrothers unamuombea Obed apone haraka ili arejee kujiunga na wenzake mapema!

0 comments:

Post a Comment

Page viewers