Subscribe:

Ads 468x60px

July 26, 2012

Azam Yafanya Kweli

Klabu ya soka ya Azam ya Tanzania bara yenye maskani yake Chamazi, leo hii imezidi kuwapa raha mashabiki wake na mashabiki wa soka wa Tanzania kwa ujumla baada ya kutinga fainali kwa kuinyuka timu ya AS Vita Club ya DRC kwa mabao 2-1.
Mabao mawili ya kipindi cha pili ya John Bocco na Mrisho Ngassa dakika za majeruhi yalitosha kuipa Azam ushindi huo baada ya kutanguliwa kwa bao moja kipindi chote cha kwanza.
Kwa Ushindi huo, Azam imetinga fainali na sasa itamsubiri mshindi kati ya Yanga na APR, mechi ambayo mpaka tunaingia mitamboni dakika ya 70, Yanga 0-0 APR.
Endelea kuwa nasi kwa matokeo kamili ya mechi za leo za nusu fainali michuano ya Kagame.

0 comments:

Post a Comment

Page viewers