Subscribe:

Ads 468x60px

October 16, 2012

Rushwa - Adui Mkubwa Wa Soka La Bongo

Hivi karibuni yametokea matokeo mengi ya kusikitisha kwenye soka letu nchini hasa kwenye Ligi yetu kuu kabisa ``Premier League`` almaarufu.
Kwanza Vilabu kugomea udhamini, kuna vilabu vilivyogomea kuvaa jezi za mdhamini mkuu wa ligi yaani Vodacom.
African Lyon, ni timu iliyomake headlines sana msimu huu baada ya kugoma kupokea jezi kutoka vVodacom zenye nembo ya Uhlsport, kampuni inachotengeneza jezi za Vodacom. hii ni kutokana na ukweli kuwa, African Lyon wameingia mkataba na kampuni ya Adidas ambao ndio wanaowatengenezea jezi zao. Ikumbukwe pia kuwa, African Lyon walizuiliwa kuvaa jezi zilizokuwa na nembo ya mshindani wa mdhamini wa ligi, Zantel. African Lyon, wamesisitiza kuuona mkataba kama sio kupata kivuli cha mkataba wa Mdhamini na T.F.F kuhusu udhamini kabla ya kupoke jezi hizo. Kwa maono yangu, African Lyon wako sahihi.
Yanga nao wameanzisha zengwe jipya baada na wao kugomea nembo ya mdhamini kwa kuwa ina rangi nyekundu na nyeupe, inayotumiwa na watani wao wa jadi Simba. Wala sitaki kulizungumzia kwa undani suala hili.
Lakini kubwa kuliko ni RUSHWA kutawala kwenye ligi yetu hii, sio tu mligi au msimu huu, bali miaka yote kumekuwa na magumashi katika uendeshaji wa ligi, vilabu hadi timu za taifa.
Juzi kati tu hapa tumeona waamuzi lukuki wakitimuliwa kutokana na kukiuka maadili ya uamuzi, unadhani chanzo ni nini....DHIKI au TAMAA au? Haieleweki!
Rushwa inatawala soka letu na tumekaa kimya, Viongozi wanahongwa, Wachezaji, waamuzi ndo balaa mpaka noma. Kwa nini? Uwajibishwaji uko wapi?
Toa maoni Yako Kuhusu Hili Tukuze Soka letu....

0 comments:

Post a Comment

Page viewers