Mdau wa Simba, Ally Shatry, Kushoto akiwa na Ezekiel Kamwaga wa Simba
Leo ndio ile siku ya Simba a.k.a Simba Day pale uwanja wa taifa ambapo Simba itatambulisha kikosi chake kipya chote kitakachoshiriki kwenye michuano ya kimataifa na ligi kuu ya msimuu huu mpya.
Leo hii, mashabiki watapata fursa ya kutambulishwa wachezaji wapya na nyota wakiwemo Mrisho Ngassa aliyetokea Azam, Mbiyu Twitte kutoka APR pamoja na kurejea kwa kipenzi chao Emmanuel Okwi. Aidha Simba mpya itamtambulisha mchezaji mwengine kutoka Azam waliyemrejesha kundini hivi karibuni kwa milioni 30, Ramadhani Chombo ''Redendo'' pale watakapocheza na timu ya City Stars ya Nairobi,Kenya mechi ya kirafiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment