Subscribe:

Ads 468x60px

August 01, 2012

Ngassa Apelekwa Simba Kwa Mkopo

Katika hali ya kushangaza na kuwashitua mashabiki wengi wa soka nchini, mchezaji aliyezua gumzo hivi karibuni ndani ya klabu yake ya Azam, Mrisho Khalfan Ngassa, amepelekwa kunako klabu ya Simba kwa mkopo.
Akithibitisha hilo, meneja wa klabu ya Azam, Patrick Kahemele alisema kuwa ni kweli wameaafikiana na klabu ya Simba kumchukua Ngassa kwa mkopo wa mwaka mmoja, ambapo klabu hiyo ya mitaa ya Msimbazi, iliridhia kulipa kiasi cha Milioni 25 na kumlipa haki zake zote alizokuwa akilipwa akiwa na Azam kwa kipindi chote atakachokuwa akiitumikia Simba. Hili limethibitishwa pia na Katibu Mkuu wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu.
Aidha katika upande wa pili wa sakata hili, Ngassa ailionekana kushangazwa na taarifa hizo na kudai kuwa hafahamu lolote kuhusu yeye kwenda Simba kwani hajaitwa na viongozi wake kulizungumzia swala hilo.Ngassa alisisitiza kuwa anachofahamu yeye ni kwamba ana mkataba na Azam anaouheshimu na hayuko tayari kuzungumzia lolote.
Lakini pia aliongeza, kama klabu yake haimtaki ni vyema wangemuambia ili wauvunje mkataba na aamue kwenda anapotaka.
Sakata hili limeibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wa soka hapa Tanzania ambapo wengi wamesikitishwa na kitendohicho walichokifanya Azam, klabu amabayo ilitegemewa kujenga taswira nzuri ya soka nchini.
Simba na Yanga zote zilikuwa zikimuwania mchezaji huyo ambapo Wanajangwani walifika dau la 20 Milioni, huku Simba wakiweka Milioni 25 mezani na hivyo kuipiku kwenye mchakato huo.

0 comments:

Post a Comment

Page viewers