Klabu ya soka ya Yanga leo imefanikiwa kulitetea kombe lake la Kgame walilotwaa mwaka jana baada ya kuifunga timu ya Azam 2-0.
Yanga ilijipatia mabao yao katika dakika za mwisho za vipindi vyote viwili kupitia kwa Hamis Kiiza kipindi cha kwanza na Said Bahanunzi kipindi cha pili na kupeleka shangwe kwa mamia wa mashabiki mitaa ya Jangwani.
Katika fainali hiyo iliyokuwa ya kusisimua na mashambulizi ya mara kwa mara kwa pande zote, Azam watajijutia wenyewe baada kukosa nafasi nyingi za wazi.
Aidha Azam watatjivunia kwa hatua kubwa waliyofikia na kuleta chngamoto mpya katika soka la Tanzania.
Azam Wamejipatia donge nono la $20,000 na Medali huku Bingwa Yanga, wamejinyakulia donge nono la $30,000 na Kombe.
Pongezi Za Dhati Kwa Yanga Kwa Kulibakisha Kombe Hili Nyumbani Na Kulitetea.
*Picha Zaidi Baada Ya Muda Mfupi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment